Kuwakaribisha

 Karibu kwenye tovuti ya maktaba ya Amilcar Cabral

Maktaba Amilcar Cabral

Juu ya Asia na Afrika na Amerika ya Kusini

Via San Mamolo 24 - 40136 Bologna (Italia)

Simu 051/581464 - faksi 051/6448034

Baruapepe: amicabr@comune.bologna.it

Wakati wa kazi ya Maktaba:

Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi: toka saa mbili na nusu asubuhi mpaka saa moja usiku;

Ijumaa na Jumamosi: toka saa mbili na nusu asubuhi mpaka saa saba na nusu asubuhi

Maktaba ya Amilcar Cabral ya Bologna inashughulika na mambo ya kimataifa na hasa siasa, jamii, uchumi na utamaduni za mataifa ya Asia, Afrika na Amerika ya Kusini. Maktaba inaandaa vipindi vya taarifa na uchambuzi (mikutano, semina, maonyesho) kuhusu mada hizo.

Maktaba ina vitabu 40.000 na magazeti 400 (majarida 50 yanaendelea kununuliwa)

Mawanda yanayoshughulikiwa ni:

 • Historia, siasa, uchumi, jamii, fasihi, utamaduni na dini za Asia, Afrika na Amerika ya Kusini;

 • Ushirikiano wa kimataifa, msaada kwa maendeleo; maingiliano ya dharura na ya huruma;

 • Mapigano na kukomeshwa kwa mapigano

 • Haki za binadamu na hali ya wanawake wa nchi zinazoendelea;

 • Maendeleo yanayoweza kuendeleza;

 • Historia ya mikutano ya Mashariki na Magharibi; vitabu vya safari;

 • Uhusiano kati ya makabila na mataifa na uhamiaji.

Maktaba ina hazina ya Afrika ya Mashariki (vitabu 800 juu ya historia na utamaduni wa Afrika, masimulizi ya safari toka karne ya 19 mpaka mwanzo wa karne ya 20, wasifu, historia kwa jumla na historia ya jeshi la Waitaliani kwenye Afrika) iliyozawadiwa na familia ya Jenerali Guerrino Lasagni.

Kuna karibu na vitabu 950 vya hazina ya Paul Sebag vinavyozungumzia habari za Tunisia na Afrika ya Kaskazini. Hapa pana vitabu juu ya elimukale, historia, elimujamii ya mji, dini, hadithi za safari, uharamia wa baharini, lugha na fasihi za kiarabu, kiebrania, jiografia.

Orodha ya vitabu vya maktaba imeingizwa kwenye katalogi ya mtandao wa mawasiliano wa kitaifa SBN na unaweza kuiona online (http://solo.cib.unibo.it:8080/SebinaOpac/Opac?sysb=UBOAI).

Huduma:

 • Makaribisho na ushauri;

 • Kukopesha vitabu;

 • Mkopo toka maktaba nyingine;

 • Uwasilishaji wa vitabu;

 • Uwekaji wa vitabu

 • Mapendekezo ya vitabu vya kununulia;

 • Kuviona vitabu;

 • Kuiona hazina ya Guerrino Lasagni;

 • Kuiona hazina ya Paul Sebag;

 • Habari za bibliografia, kwa baruapepe (amicabr@comune.bologna.it), kwa simu (051581464), kwa BiblioChat na huduma ya marejeo online inayoitwa "Chiedilo al bibliotecario" (maana yake ni "Mwulize mkutubi") (http://www.centrocabral.com/adon.pl?act=doc&doc=338);

 • Kusoma magazeti na majarida;

 • Fotokopi;

 • Kuiona katalogi online;

 • Mahali pa kusoma;

 • Kompyuta inayowezesha kutafuta kwenye mtandao;

segnalazioni